UJASILIAMALI MDOGO NACHINGWEA.


KIKUNDI CHA WANAWAKE WAJANE NA WANAWAKE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
UTANGULIZI
Katika kuguswa na jamii pamoja na maisha ya kila siku ya wanawake wajane ndio kulikopelekea kikundi cha NISHIKE MKONO kuanzishwa kikiwa na lengo kuu la kuwafanya wanawake wajane wajikwamue kiuchumi na kuwafanya wasiteteleke hasa baada ya kuondokewa na wenzi wao ambao kwa kiasi kikubwa ndio walikuwa tegemeo katika maisha yao ya kila siku. Hii ni kutokana na wanawake wengi kuwa mama wa nyumbani wakati waume zao wakiwa ndio nguzo ya familia kwa mahitaji yote muhimu kama vile kusomesha watoto, chakula na mambo yote ya kifamilia.
NAMBA
JINA LA MWANACHAMA
CHEO
1
HAMISI KAMBONA
MWENYEKITI/MWEZESHAJI UJASILIA MALI
2
MWAJUMA ALLY DADY
KATIBU
3
ANIFA MPILI
MWEKA HAZINA
4
ZAINABU ABASI
MWANACHAMA
5
ELIZABERTH STAMBULI
MWANACHAMA
6
MARISELA JACKSON PETER
MWANACHAMA
7
STELA KIMBUNGA
MWANACHAMA
8
SAKINA MAPUNDA
MWANACHAMA
9
SHAKILA LIBABA
MWANACHAMA
10
BINADA MAKWALILO
MWANACHAMA
11
SCOLASTICA MJUMBA
MWANACHAMA
12
CHAUSIKU MSHANGANI
MWANACHAMA
13
MARIAMU CHINGUILE
MWANACHAMA
Kikundi kilianzishwa mwaka mwezi julai 2018 kikiwa na jumla ya wanachama 13 ambao wamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kundi la uongozi na ushauri na kundi la wanachama wajane. Kama yaliyoainishwa hapa chini katika jedwali lifuatalo;

MALENGO YA KIKUNDI
Malengo ya kikundi cha NISHIKE MKONO MJANE yamegawanyika katika makundi matatu yote yakiwa na umuhimu unaolenga kumuinua mjane ili aishi kama mwanzo na kumuondolea upweke na mawazo na kumfanya shupavu na mwenye nguvu. Malengo haya ni kama yafuatayo hapa chini.
1.       Kuinuana kiuchumi.
Kuinuana kiuchumi ni moja kati ya malengo ya kikundi chetu, ambapo wakati tunaanzisha kikundi chetu ni baada ya kuvunja kikundi cha vikoba ambapo akina mama walipata pesa ndogo sana ambayo isingeweza kuwasaidia kwa lolote kwasababu pesa waliyokuwa wakichangia ni ndogo sana. Hapo ndipo lilipopatikana wazo a kuunda kikundi cha wajane cha kusaidiana.
Kama wamama wajane tulichanga pesa kidogo na kuanziasha biashara ndogo ya kupika maandazi kwa kuwekeana zamu na pesa kuzitunza kidogokidogo. Pesa ilipoongezeka kiasi tulianza kukopeshana wenyewe kwa mtu aliyekuwa na wazo la biashara.
2.       Kupeana elimu na uzoefu katika ujasilia mali.
Kikundi kina lengo la kupeana uzoefu na elimu ya ujasilia mali. Kikundi kimedhamilia kutoa elimu ya jinsi ya kuthubutu na kuzitumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi. Tumekuwa tukipata elimu ya ujasilia mali kwa wajasiliamali wenzetu na kupeana uzoefu mbalimbali ambao umetujengea uwezo  na kuwa majasili wa kuzitumia fursa.
3.       Kufarijiana na kushauriana katika maisha.
Lengo la tatu la kikundi chetu ni kufarijiana na kupeana matumaini hasa pale mtu anapokosa matumaini na kukata tamaa kabisa. Wapo wenzetu waliobobea katika kutoa elimu ya ushauri nasaa na kufarijiana hasa wakati wa shida kama vile ugonjwa, mawazo, madeni na n.k.
MAFANIKIO YA KIKUNDI
Kikundi kimepata mafanikio kiasi pamoja na changamoto nyingi tunazozipitia kila siku katika kukiendeleza kikundi chetu. Pamoja na mazuri tuliyoyafanya na kupata, yafuatayo tunajivunia
1.       Tumeanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji katika banda letu dogo tuliloliazima kutoka kwa mwanakikundi mwenzetu. Una jumla ya kuku 50 wakiwemo makoo 40 na majogoo 10 ambao tumeanza nao kwa kuwanunua kwa jumla ya shs 500000 kwa bei @ 10000/=. Wameanza kutaga mayai tayari. Pia tuna bata 10 ambao kila mwanakikundi alileta kutokana na mkakati wetu tuliojiwekea na katiba ya kikundi chetu.
2.       Tumefanikiwa kununua kiwanja ambacho nia na malengo yetu tujenge ofisi zetu za ujasilia mali za kikundi ili kurahisisha mikutano na shughuli zetu kukwepa hali ya sasa ya kukutana nyumbani kwa mtu. Hii itasaidia kukikuza kikundi chetu na kufanya watu na jamii inufaike na kile tunachokifanya. Kiwanja chetu kina ukubwa wa square mita 450 ambacho kitatosha kwa kazi zetu kwa sasa.
3.       Tuna ratiba ya kukutana kila siku ya jumapili ili kukaa pamoja na kujadiliana na kupeana ushauri wa baadhi ya mambo na changamoto, achilia mbali siku za kukutana za kawaida za kikundi ambazo ni jumatano na jumamosi kwa jumla pamoja na kila siku kwa wale wenye ratiba katika kikundi chetu hasa zile za kuwahudumia kuku.
4.       Tunatoa mikopo isiyo na riba kwa wamama wajane ambao ndo walengwa, pia tunatoa mikopo kwa wamama wengine ambao sio wanachama kwa riba ya 5% ili kuhamasisha akina mama wajiunge katika kikundi chetu ili wanufaike na kikundi hiki pamoja na kuongeza mtaji wa kikundi chetu.
CHANGAMOTO
Kama kikundi tuna changamoto nyingi zinazotukabili ambazo zinatufanya kasi yetu katika kikiendeleza kikundi kupungua na kutaka kupunguza nguvu kwa wanachama. Zipo tulizokabiliana nazo na zile zinazotushinda kuzitatua kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi wa kikundi chetu. Changamoto hizi tumezigawa katika makundi matatu kama zinavyofafanuliwa hapa chini
(a)    Mtaji mdogo
Tuna mtaji mdogo wa kuendesha kikundi kiasi ambacho kuna wakati mwanakikundi anaweza kuhitaji mkopo na asipate kwa wakati mpaka muda wa marejesho kwa mwanachama mwingine aliyeazima pesa anaporudisha ndio unakuwa wasaa wa mtu mwingine kuchukua mkopo, tena kwa kiwango kisichokidhi mahitaji yake ya mkopo kwa wakati huo, hali inayofanya malengo ya wanachama yasitimie katika ujasiliamali wetu.
(b)   Mapokeo ya jamii
Kwakuwa kikundi hiki ndio kinaanza, tunakutana na changamoto ya kutopokelewa vizuri katika jamii kutokana na wingi wa vikundi vingi vilivyoanzishwa visivyokuwa na tija wala malengo sahii ndani ya jamii. Tunakabiliana nazo changamoto hizi kwa kufanya kazi kwa bidii ili waaminishwe na mafanikio yetu hapo baadae kama malengo na matarajio yetu yalivyo na ukomavu wetu wa kupambana na changamoto nadani ya kikundi chetu. Tunaamini siku moja jamii itatuelewa nini tunafanya na nini hasa malengo ya kikundi chetu.
(c)    Mfumo dume
Changamoto nyingine ni mfumo dume ambao unapelekea wababa wengi kuona aibu kuja kukopa kwenye kikundi chetu wakiamini kama hatuwezi kuwakopesha japo kidogo na kutudharau hasa pale tunavyotoa elimu ndogo kwa wajasiliamali ambao wameanza kuona mafanikio yetu na kuwa na mitazamo ya mbali yenye mafanikio.
MAHITAJI YA KIKUNDI
Kama kikundi tunaomba msaada wa kiasi cha pesa cha Tshs 10047500/= sawa na dollor 4067.814 za kimarekani ili kukiendeleza kikundi chetu kichanga kama mchanganuo wa matumizi yafuatayo kwenye jeduali hapa chini.
AINA YA MATUMIZI
MCHANGANUO
KIASI (TSHS)
KIASI (USD)
KUONGEZA MRADI WA KUKU
1120000
453.4413
KUNUNUA MADAWA NA CHANJO
6KG @ 30000
180000
72.87449
VYOMBO VYA CHAKULA NA MAJI
20 PC@15000
300000
121.4575
POSHO YA MTAALAMU WA UJASILIAMALI
SIKU 4/MWEZI @ 15000
720000
291.498
POSHO YA MLINZI WA BANDA
1 @ 50000/MIEZI 12
600000
242.915
GHARAMA ZA UENDESHAJI WA KIKUNDI
MATUMIZI  MADOGO
100000
40.48583
MIKOPO KWA WAMAMA
25 @ 200000
5000000
2024.291
BIMA ZA AFYA YA JAMII (CHF)
20 @ 15000
300000
121.4575
VITAMBULISHO VYA WAJASILIA MALI
20 @ 20000
400000
161.9433
VITABU VYA KUMBUKUMBU
90000
36.43725
VIFAA VINGINE
10000
10000
4.048583
UKARABATI WA BANDA



1. KUWEKA TAA KUBWA
5 @5000
25000
10.12146
2. GHARAMA ZA WAYA
MITA 15 @ 3500
52500
21.25506
3. FUNDI UMEME
1 @ 150000
150000
60.72874
AKIBA YA KIKUNDI
DHARULA
100000
404.8583

JUMLA KUU
10047500
4067.814




UWAJIBIKAJI NA KUKIKUZA KIKUNDI CHETU
Kama kikundi tumejizatiti kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yetu, hivyo tunatarajia kufanya mambo makubwa ambayo yatakuwa mfano wa kuigwa katika jamii yetu inayotuzunguka na ikiwezekana hata Taifa kwa ujumla. Tunaamini tutakuwa mfano wa kuigwa na kioo bora kwa jamii kitakachowavutia wajane wengi kujiunga na sisi na kuwakwamua kiuchumi zaidi.
HITIMISHO
Tunatanguliza shukurani zetu za dhati,

HAMISI KAMBONA
MWENYEKITI KIKUNDI CHA WAJANE CHA NISHIKE MKONO
NACHINGWEA-LINDI.
0714427055

Comments

Popular posts from this blog

NDOTO ZANGU