Posts

Showing posts from 2018

Kizaa zaa!!!

Sikuwahi kuwaza hata siku moja kama nitalala sello kama mtuhumuwa! Kwa kweli mwaka 2018 niliuanza vibaya pale jengo la shule lilipoungua na kuteketea kwa moto. Siku 4 ndani!!!!! Nimejifunza yafuatayo:- 1. Kuna maisha mengine zaidi ya haya tunayoishi kila siku. 2. Kuna watu wana shida zaidi ya hizi tuzionazo kwa macho au maisha ya kawaida. 3. Hakuna tofauti kati ya asubuhi na jioni, mwanga ni uleule. 4. Ukiwa karibu na kitu kinachotoa harufu kwa muda mrefu huwa kunabadirika na kunukua. 5. Usingizi unakuja hata ukuwa kwenye maji au dimbwi la matatizo. 6. Hakuna mtu anakukumbusha deni lake ukiwa sello. 7. Kuoga ni option. 8. Milio tisa ya mbu na tamaduni zao. Natamani 2018 ipite fastaaa!!!!!